Mbunge John Waluke, Grace Wakhungu huru

0

Mbunge wa Sirisia John Waluke pamoja na mshtakiwa mwenza Grace Wakhungu wamepata afueni baada ya mahakama kuwaachilia kwa dhamana.

Waluke na Wakhungu wameachiliwa kwa dhamana ya Sh10M na Sh20 mtawalio baada ya mahakama kuridhia ombi lao la kuachiliwa kwa dhamana wakisubiri rufaa yao kusikilizwa.

Wawili hao walikuwa wamefungwa jela miaka 67 na 69 mtawalia baada ya kupatikana na hatia kwenye sakata ya mahindi ya shilingi Sh313M katika shirika la nafaka na mazao NCBP.

Waluke alihukumiwa miaka 67 jela au alipe faini ya Sh1b huku Wakhungu akihukumiwa miaka 69 jela au alipe faini sawa na hiyo.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here