Kamati ya bunge la kitaifa kuhusu usalama imewasuta wendani wa naibu rais William Ruto kutokana na kile imetaja kama kueneza porojo kuhusu awamu ya pili ya kuwasijili Wakenya kupitia Huduma Namba.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Paul Koinange anasema bunge liliidhinisha bajeti ya zoezi hilo na kwamba watazunguka kote nchini kuwafahamisha Wakenya kuhusu usajili huo ili kuwaepusha na uongo kutoka kwa wendani wa Ruto.
Aidha wanachama wa kamati hiyo wamemtaka naibu rais kujiuzulu badala ya kupinga mipango ya serikali ilhali yuko ndani ya hiyo serikali.