Mgonjwa mmoja anaarifiwa kufariki katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta kufuatia mgomo wa wafanyikazi ulioanza leo.
Inaripotiwa kuwa marehemu alifariki akiwa katika eneo la kuegesha magari la hospitali hiyo kwani hakukuwa na mhudumu wa kumshughulikia.
Wagonjwa wengine wamelazimika kutafuta matibabu kwingineko baada ya kusubiri bila mafanikio kutibiwa katika hospitali hiyo.
Wahudumu hao wakiongozwa na Albert Njeru wanalamikia kutolipwa nyongeza ya mishahara waliyofaa kupewa baada ya hadhi ya hospitali hiyo kupandishwa.
Katibu mkuu wa muungano wa wauguzi nchini KNUN Seth Panyako alihudhuria maandamano hayo ameishtumu tume ya kutathmini mishahara ya watumishi wa umma SRC kwa kupinga nyongeza hiyo.
Wafanyikazi hao ikiwemo madaktari na wauguzi wamesema hawatarejea kazini iwapo mishahara yao haitaongezwa.