Mbunge wa Homa Bay Mjini, Peter Kaluma, ametilia shaka hatua ya aliyekuwa Jaji Mkuu, David Maraga, kufika mahakamani kumuunga mkono mwanaharakati, Rose Njeri.
Kupitia kwa taarifa, Kaluma ameeleza wasiwasi wake kuhusu ushiriki wa Maraga katika kesi hiyo, akisema hatua hiyo huenda ikaathiri mtazamo wa umma kuhusu urithi wa uongozi wa Jaji huyo mstaafu.
Mbunge huyo pia amesisitiza wito wake kwa serikali kuanzisha njia rasmi za kuwahusisha maafisa wakuu wa serikali waliostaafu katika shughuli za kitaifa.
Jaji Maraga, ambaye tayari ametangaza azma yake ya kuwania urais mwaka 2027, ameendelea kuzuru maeneo mbalimbali ya nchi kueneza ujumbe wa kisiasa kuhusu nia yake.
Anatarajiwa kutangaza chama cha kisiasa atakachokitumia katika kampeni zake katika miezi ijayo, wakati akijipanga kumrithi Rais William Ruto.









