Mashirika yakashifu ongezeko la mimba za utotoni

0

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameitaka serikali kuchukua hatua madhubuti kukabili ongezeko la visa vya mimba za utotoni nchini.

Kudhibiti unyanyasaji wa kijinsia na kulinda watoto walio katika mazingira hatari ni baadhi ya hatua ambazo mashirika hayo yalilitaka bunge la seneti kuchukua.

Msukumo huo unafuatia ripoti tata kutoka kwa idara ya jinsia kaunti ya Lamu iliyoonyesha kuwa eneo hilo lilirekodi visa 1,073 vya mimba za utotoni kati ya mwaka wa 2024 na Mei 2025.

Kati ya hivi, visa 789 vilitokea mwaka uliotangulia na 284 vikirekodiwa kati ya Januari na Mei 2025.

Ripoti hiyo iliwasilishwa kwa Kikosi Kazi kilichobuniwa na rais William Ruto chini ya uongozi wa Nancy Barasa kuhusu unyanyasaji wa kijinsia, ikijumuisha mauaji ya wanawake.

Shirika la Muhuri, ambalo pia liliwasilisha matokeo yake kwa jopo kazi, lilisema mimba nyingi zilitokana na ubakaji, unajisi na ndoa za utotoni-maswala yanayoashiria mapungufu katika mifumo ya haki.

Kulingana na baraza la kitaifa la kudhibiti magonjwa ya syndemic, wastani wa wasichana 696 walipachikwa mimba kila siku mnamo 2023.

Mwaka uliopita, KHRC iliorodhesha kaunti 10 zilizokuwa na viwango vya juu zaidi vya mimba za utotoni kati ya wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 19.

Kaunti hizo ni pamoja na Nairobi, Bungoma, Nakuru, Machakos, Kiambu, Kakamega, Meru, Kilifi, Narok na Kisii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here