MAGAVANA WAUNGA MKONO PESA ZA NYUMBA ZA BEI NAFUU KUJENGA MASOKO

0
GAVANA ABDULLAHI

Baraza la Magavana (CoG) limeunga mkono hatua ya serikali ya kutumia fedha za ushuru wa nyumba za bei nafuu kufadhili si tu ujenzi wa nyumba, bali pia miundombinu muhimu ya umma kama vile masoko.

Mwenyekiti wa baraza hilo, Ahmed Abdullahi, ambaye pia ni Gavana wa Wajir, amesema kuwa baraza hilo linaunga mkono tafsiri pana ya mpango wa makazi, ili kujumuisha miundombinu inayosaidia kujenga jamii zenye mazingira bora ya kuishi na zinazojumuisha wote.

Amefafanua kuwa magavana walifanya kikao cha kina na Rais Ruto wiki iliyopita, ambapo walikubaliana juu ya umuhimu wa kujumuisha huduma za kijamii katika mpango huo wa makazi.

Haya yanajiri wakati ambapo Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi (COTU) umekosoa hatua hiyo, ukionya kuwa kutumia ushuru huo kwa miradi zaidi ya ujenzi wa nyumba huenda kukawa ni kinyume cha sheria.

Katibu Mkuu wa COTU, Francis Atwoli, ameonya kuwa kupanua matumizi ya ushuru huo kupita mipaka ya kisheria kunaweza kusababisha matumizi mabaya ya fedha, akisisitiza kuwa ushuru huo unatakiwa kutumika tu kwa ujenzi wa nyumba.

Hata hivyo, serikali imesisitiza kuwa mpango wa nyumba za bei nafuu unahusisha zaidi ya ujenzi wa nyumba pekee, na kujumuisha kuendeleza makazi yaliyopangiliwa kwa njia ya kuunganisha huduma muhimu za kijamii kwa wakazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here