Mwanamme mmoja amehukumiwa kifo na Mahakama ya Kibera baada ya kupatikana na hatia ya kuiba simu ya rununu katika eneo la Kawangware, Nairobi.
Mwanamme huyo kwa jina Isaac Khanga amepatikana na hatia ya kuwaibia wanaume wawili simu za dhamani ya shilingi elfu 39 na shilingi elfu 30 pesa Taslim mnamo tarehe tatu Novemba mwaka jana katika eneo la Madiaba.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, Khanga Pamoja na washukiwa wengine ambao hawakuwa mahakamani aliiba simu aina ya Tecno ya dhamani ya shilingi elfu 24 na shilingi elfu 30 pesa Taslim katika kisa cha kwanza kabla ya kuiba simu ya dhamani ya shilingi elfu 15 katika kisa cha pili.
Akitoa uamuzi huo, hakimu mkuu Christine Njagi amesema hukumu ya kifo ingali halali nchini kwani haijatangazwa kuwa kinyume cha sheria.









