Matiang’i atangaza kafyuu ya kutotoka nje yawekwa Kapedo

0

Serikali itaweka amri ya kutotoka nje kati ya saa kumi na mbili jioni hadi saa kumi na mbili asubuhi katika eneo la Kapedo kama njia mojawapo ya kuimarisha usalama katika eneo hilo.

Waziri wa usalama wa ndani Dr Fred Matiang’i amesema kafyu hiyo itawawezesha maafisa wa usalama kuwanasa wahalifu wanaowahangaisha wakaazi n ahata kusababisha maafa.

Oparesheni ya kiusalama inaendelea katika eneo hilo la Kapedo kufuatia kuuawa kwa afisa mmoja wa GSU na wengine wawili kujeruhiwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here