Madai ya Sonko kuhusu ghasia za 2017 yazua tumbo joto

0

Chama cha ODM kinataka asasi husika za serikali kuchunguza madai yaliyotolewa na gavana wa Nairobi aliyetimuliwa Mike Sonko kuhusu ghasia za uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.

Kupitia katibu wake mkuu Edwin Sifuna, ODM inataka uchunguzi kamili kufanywa na iwapo itabainika kuwa ni ukweli, wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.

Sonko alidai kwamba yeye pamoja na baadhi ya maafisa wa ngazi za juu serikalini walipanga njama ya kuzua ghasia baada ya uchaguzi huo ili kukifanya chama cha ODM kuonekana kibaya mbele ya Wakenya.

Awali, katibu katika wizara ya usalama wa ndani Karanja Kibicho alijiwasilisha katika makao makuu ya idara ya jinai DCI kuandikisha taarifa kuhusiana na madai hayo.

Kibicho ni miongoni mwa waliotajwa na Sonko kwa kuhusika kwenye njama hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here