Muungano wa matabibu nchini (KUCO) umemtaka rais Uhuru Kenyatta kupiga marufuku mikutano yote ya kisiasa kwa kuchangia katika msambao wa virusi vya corona.
Wakiongozwa na katibu mkuu George Gibore, matabibu wanawashutumu wanasiasa kwa kupuuza masharti ya usalama na kuendelea mbele na mikutano ya kuomba kura pasipo kujali hatari ya ugonjwa huo.
Muungano huo aidha umetoa tahadhari kwamba maambukizi mapya ya ugonjwa huo yameilemea nchi huku hospitali zikijaa wagonjwa wa corona.