DCI wasema walipata pesa za hongo kwa majaji wawili walioshikwa

0

Wapelelezi wa DCI sasa wanasema walipata Shilingi Milioni sita kwenye afisi za majaji wawili waliokamatwa juma lililopita kwa tuhuma za ufisadi.

Kwenye hati kiapo iliyowasilishwa mahakamani, DCI kupitia Inspekta mkuu Felix Banzi imeambia mahakama kwamba walipata zaidi ya shilingi milioni tano kutoka kwa mwanamke mmoja aliyekuwa kwa chumba cha Jaji Aggrey Muchelule na shilingi zaidi ya laki saba kutoka kwa Jaji Said Chitembwe.

DCI wanaamini kwamba pesa hizo zilikusudiwa kumlambisha hongo jaji mmoja ambaye jina lake halijafichuliwa.

Wapelelezi walipekua vyumba vya wawili hao kwenye msako wiki iliyopita kabla ya kuwashika na kuwapeleka hadi katika makao makuu ya DCI ambapo walihojiwa.

Wakili wao Danstan Omari alisema kuwa wapelelezi hawakupata hata peni moja wakati wa msako huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here