Maseneta wamewashutumu magavana kwa kusimamia wizi wa pesa katika serikali za kaunti.
Wakiongozwa na seneta wa Kakamega Cleophas Malala, maseneta wamewatuhumu magavana kwa kuzifilisi kaunti kupitia kukiuka sheria na kufumbia macho ubadhirifu wa pesa zilizofaa kutumika kufanikisha ugatuzi.
Baadhi ya magavana wanadaiwa kuiba pesa za kaunti ili kutumia kwenye uchaguzi mkuu wa 2022 huku wengine wakitoa zabuni kwa kampuni wanazohusishwa nazo.
Yanajiri haya huku kamati ya bunge hilo la Senate kuhusu Uhasibu chini ya uenyekiti wake Seneta wa Migori Achilo Ayacko likimhoji Gavana wa Pokot Magharibi Prof. John Lonyangapuo kuhusu matumizi ya pesa za mwaka 2018/2019.