Mbunge wa Bonchari John Oroo Oyioka atazikwa Ijumaa wiki ijayo nyumbani kwake Suneka kaunti ya Kisii.
Mwenyekiti wa kamati ya mazishi ya mwendazake Geoffrey Mogire anasema ibada ya wafu itaandaliwa siku iyo hiyo katika shule ya upili ya Iteirerio.
Mogire ameongeza kuwa hafla ya kuchangisha pesa kwa ajili ya mazishi itaandaliwa Jumanne wiki ijayo katika hoteli moja jijini Nairobi na nyingine nyumbani kwake Suneka.
Oroo alifariki kutokana na ugonjwa Kiharusi katika hospitali ya Aga Khan, Kisumu.