Kwa nini MCAs walipewa mikopo ya magari wakati huu? NCCK yauliza

0

Baraza la makanisa nchini (NCCK) limetilia shaka hatua ya serikali kuwapa madiwani mikopo ya kununua magari wakati ambapo mjadala wa kuidhinisha mswada wa marekebisho ya katiba BBI unaendelea katika mabunge ya kaunti.

NCCK katika taarifa inasema licha ya kuwa huenda hatua hiyo ilikuwa na nia njema, wakati ambapo mikopo hiyo imetolewa unaibua maswali kwa sababu upo uwezekano kwamba madiwani watashashiwika kupitisha mswada huo mradi tu wapate mikopo hiyo wanunue magari.

Baraza hilo vile vile limetoa changamoto kwa mabunge ya kaunti kuhusisha umma kikamilifu kabla ya kufanya uamuzi kuhusu hatma ya mswada huo.

Aidha, katibu mkuu wa baraza hilo Chris Kinyanjui ameitaka serikali kuweka mikakati inayofaa ikiwemo kuwateua makamishna wapya wa IEBC taifa linapojiandaa kwa kura ya maamuzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here