Mama akamatwa Mlolongo kwa kujaribu kuuza mtoto

0

Mwanamke mmoja amekamatwa kwa madai ya kujaribu kumuuza mwanawe mchanga katika eneo la Mlolongo, kaunti ya Machakos.

Naibu kaunti kamishna wa Mlolongo Dennis Onganga anasema mwanamke huyo alikuwa anajaribu kumuuza mwanawe kwa Sh60,000.

Mwanamke huyo amedai kuwa alikuwa anapania kumuuza mwanawe kwa sababu ya changamoto za kifedha.

Cheti cha mtoto kuzaliwa kinaonesha kuwa alizaliwa September 2 katika hospitali ya Machakos Level 5.

Mama huyo anazuiliwa katika kituo cha Polisi cha Mlolongo huku mtoto huyo akipelekwa katika kituo cha Mahali pa Maisha Rescue Home.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here