Watu 1,068 wakutwa na corona, 12 wafariki

0

Kenya kwa mara ya kwanza imeandikisha idadi kubwa ya visa vya ugonjwa wa corona kwa siku moja baada watu 1,068 kukutwa na ugonjwa huo kati ya sampuli 7,556 zilizopimwa

Watu hao wanaojumuisha mtoto wa miezi sita ni Wakenya 1,044 na raia 24 wa kigeni.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema hii inafikisha 47,212 idadi ya visa hivyo nchini kufikia sasa.

Nairobi inaongoza kwa kuandikisha visa 305 ikifuatiwa na Nakuru ilio na visa 137, Mombasa 74, Kisumu 60 na Kericho 58.

Wagonjwa wengine 12 wamefariki na kufikisha 870 idadi ya maafa yanayotokana na ugonjwa huo.

Idadi ya waliopona imeongezeka na kufikia 33,050 baada ya watu 290 zaidi kupona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

27 ndio idadi ya wagonjwa walio kwenye chumba cha watu hali mahututi ICU, 47 kati yao wakisaidiwa na mashine kupumua.

Wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali ni 1,121 huku wanaoshughulikiwa nyumbani wakiwa 3,112.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here