Shule za kimataifa hazitafunguliwa Jumatatu

0

Shule za kimataifa zimesitisha mipango ya ufunguzi wa shule hizo kwa awamu ya pili Jumatatu ijayo ambayo ni Octoba 26 kufuatia kuongezeka kwa visa vya ugonjwa wa corona.

Katika arifa, muungano wa shule hizo hapa nchini umesema uamuzi huo umesababishwa na kuendelea kuongezeka kwa visa vya ugonjwa huo.

Shule hizo zilirejelea masomo kufuatia hatua ya wizara ya elimu kufungua shule Octoba 12 kwa wanafunzi wa darasa la nne, darasa la nane na kidato cha nne.

Muungano huo ulitarajia kuwaruhusu wanafunzi zaidi kuripoti shuleni ila sasa uamuzi huo umetiwa breki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here