MAKANISA YASHINIKIZA SERIKALI KURUHUSU MAANDAMANO YA AMANI

0

Muungano wa Huduma za Kanisa nchini (KCCAM) umetoa matakwa matatu kwa serikali kuhusu kifo cha mwalimu Albert Ojwang.

Katika taarifa bodi kuu ya KCCAM imeitaka Mamlaka ya kuangazia utendekazi wa maafisa wa Polisi (IPOA) kuharakisha uchunguzi wake kuhusu kifo cha Ojwang na kesi zingine ambazo hazijatatuliwa.

Kanisa pia limemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi kuhakikisha maafisa kote nchini wanaruhusu maandamano ya amani kuendelea bila kuingiliwa.

Muungano huo pia umemtaka Rais William Ruto kuchukua jukumu kuu katika kuthibitisha kuwa mamlaka ya usalama ni ya kuwalinda Wakenya.

Aidha wamesema kuwa kifo cha Ojwang, pamoja na visa vingine vilivyoripotiwa vya kutumia nguvu kupita kiasi, vimeathiri imani ya umma kwa taasisi za usalama.

Ojwang alifariki akiwa chini ya ulinzi wa polisi chini ya hali tatanishi ambayo bado haijafahamika.

Kifo chake kilizua maandamano, haswa jijini Nairobi, huku waandamanaji wakidai majibu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here