Mabunge zaidi yazidi kupitisha mswada wa BBI

0

Mabunge ya kaunti ya Turkana, Kericho na Wajir yamekuwa ya hivi punde kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba BBI na kufikisha 41 idadi ya kaunti zilizopitisha mswada huo.

Katika bunge la kaunti ya Wajir, madiwani wamepitisha mswada huo kwa kauli moja wakihoji kwamba kaunti zitafaidika zaidi kupitia kwa pesa nyingi kutumwa mashinani.

Madiwani wa bunge la kaunti ya Kericho walitofautiana ile walipiga kura kura ya kuunga mkono mswada huo walishinda.

Kaunti zingine zilizopitisha mswada huo ni ile ya Tharaka Nithi, Kirinyaga, Nakuru, Meru, Nyandarua, Mombasa, ikifuatwa na Garissa, Lamu, Machakos, Nyeri na Kitui.

Vilevile kaunti za Muranga, Bungoma, Taita Taveta, Nyamira, Makueni, Narok na Kakamega zimepitisha mswada huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here