Kenya imeripoti visa vipya 280 vya corona baada ya kupima sampuli 4,919 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.
Hii inafikisha 104,780 idadi ya visa vya ugonjwa huo vilivyodhibitishwa nchini kufika sasa.
Habari njema ni kwamba watu wengine 713 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 86,378.
Idadi ya maafa imeongezeka na kufikia 1,839 baada ya wagonjwa 2 zaidi kufariki.
Wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali kwa sasa ni 344 huku wengine 1,495 wakishughulikiwa nyumbani.