MAASKOFU WA AIC WAKUTANA NA RAIS RUTO

0

Askofu mkuu wa kanisa la Africa Inland Church (AIC) Abraham Mulwa amewaongoza maskofu wengine katika kukutana na Rais William Ruto.

Katika mkutano huo kwenye Ikulu ya Nairobi, kiongozi wa taifa ametaja umuhimu wa kanisa katika jamii.

“Kanisa linasalia kuwa nguzo na ngome imara ya maadili, utu, na nguvu ya kiroho,”amesema Rais Ruto.

Rais Ruto ameongeza serikali na mashirika ya kidini hushirikiana pia katika utoaji wa huduma za afya na elimu, pamoja na majukumu mengine ya kibinadamu.

Mkutano huo umewaleta pamoja maaskofu wa AIC wa humu nchini na wengine kutoka Tanzania, Sudan Kusini, Rwanda DRC Kongo na London.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here