Maafa ya COVID19 yafikia 311

0

Idadi ya maafa kutokana na ugonjwa wa corona nchini Kenya imeongezeka na kufikia 311 baada ya wagonjwa 12 kufariki katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe aidha amedhibitisha kuwa watu 544 wamepatikana na ugonjwa huo na kufikisha idadi ya visa hivyo nchini kuwa 19,125.

Msambao wa visa hivyo ni kama ifwatavyo; Nairobi 326, Kiambu 51, Kajiado 33, Nakuru 20, Busia 19, Mombasa 15, Machakos 11, Narok 10, Uasin Gishu, Murang’a & Migori 9, Kisii 7, Laikipia 6, Nyeri 5, Kisumu 4, Bungoma 2, Kericho, Kakamega, Homabay, Nyamira, Nyandarua, Trans Nzoia, Vihiga na & Pokot 1.

Idadi ya waliopona imeongezeka na kufikia 8,021 baada ya wagonjwa 113 kupona.

Jijini Nairobi, msambao wa visa hivyo ni kama ifwatavyo; Westlands 35, Embakasi East 31, Kasarani 27, Kibra 26, Makadara 24, Dagoreti North 23, Embakasi West 23, Roysambu 18, Embakasi North 17, Kamukunji & Langata 16, Dagoreti South, Embakasi South & Starehe 14, Ruaraka 12, Embakasi Central 11 & Mathare 5.

Wakati uo huo

Takriban wahudumu wa afya 634 wameambukizwa virusi hatari vya corona wakiwa kazini.

Hii ni kulingana na waziri wa afya Mutahi Kagwe ambaye hata hivyo amewalaumu baadhi ya madaktari kwa kupuuza vigezo muhimu vya usalama ili kuepuka maambukizi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here