Polisi atuhumiwa kumbaka mwanamke kwenye karantini Busia

0

Afisa wa magereza anazuiliwa kwa tuhuma za kumbaka mwanamke ambaye amekuwa kwenye karantini katika kituo cha mafunzo ya Kilimo kaunti ya Busia mapema leo asubuhi.

Emmanuel Ngetich ambaye anahudumu katika gereza la Busia ni miongoni mwa maafisa sita ambao wanalinda watu kwenye karantini hiyo na anadaiwa kumhadaa mwanamke huyo kabla ya kumtemdea unyama huo.

Afisa mwenzake anasema walikuwa kwenye patroli jana usiku lakini akabaki nyuma akishauriana na mwanamke huyo kwa muda mrefu na akaenda kuwapasha habari wenzake.

Maafisa wengine walipofika walipata watu wengine waliokuwa wametengwa pia kwa kuhofiwa kuwa na virusi vya corona walikuwa nje na walipoulizwa wakasema chanzo ni unyama uliokuwa ukiendelea katika chumba cha mmoja wao.

Afisa huyo tayari amenyanganywa bunduki yake na uchunguzi umeanzishwa kabla ya mshukiwa kufikishwa mahakamani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here