Ijumaa ni siku kuu – Matiang’i

0

Waziri wa Usalama wa ndani Dkt. Fred Matiang’i ametangaza Ijumaa Julai 31 kuwa siku kuu.

Siku hiyo itakuwa siku kuu kuadhimisha sherehe za Idd-ul-Azha ambayo ni siku muhimu katika kalenda ya waumini wa dini ya Kiislamu.

Waziri Matiangi katika chapisho rasmi la serikali amewataka waumini hao kuzingatia masharti ya usalama kuepuka msambao wa corona wakati wa maadhimisho hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here