Kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa corona nchini kimefikia asilimia 13.2% baada ya taifa kuandikisha visa 965 kati ya sampuli 7,311 zilizopimwa katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema hii inafikisha 153,488 idadi ya maambukizi ya ugonjwa huo nchini kufikia sasa.
Idadi ya waliopona imefikia 105,279 baada ya kupona kwa watu wengine 1,441 huku maafa yakifikia 2,540 baada ya kufariki kwa wagonjwa 21 zaidi.
Haya yanajiri huku magavana wakidai kwamba Kenya inaandikisha idadi ndogo ya maambukizi mapya kwa sababu hakuna vifaa vya kuwapima watu.
Kupitia kwa taarifa, mwenyekiti wa kamati ya afya ya katika baraza la magavna Profesa Anyang’ Nyong’o amesema serikali za kaunti hazina vifaa hivyo na kuitaka wizara ya afya kuchukua hatua za haraka.