Kilifi yapitisha BBI

0

Bunge la kaunti ya Kilifi limekuwa la hivi punde kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba BBI.

Madiwani wa bunge hilo wamepitisha mswada huo kwa kauli moja.

Kaunti hiyo sasa imekuwa ya 42 kupitisha mswada huo.

Hayo yanajiri siku moja baada ya bunge la kaunti ya Nandi kuwa la pili kuangusha mswada huo baada ya bunge la kaunti ya Baringo.

Wabunge wanatazamiwa kuanza kuujadili mswada huo wiki ijayo baada ya kupokea dhibitisho kutoka kwa mabunge yaliyopitisha mswada huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here