Mahakama yawazuilia washukiwa wawili wa mauaji ya Wanjiru

0

Washukiwa wawili wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya mfanyibiashara Caroline Wanjiku watazuiliwa kwa siku kumi zaidi kuwaruhusu Polisi kukamilisha uchunguzi.

Uamuzi wa kuendelea kuwazuilia wawili hao Edwin Otieno na Samwel Okoth umetolewa na mahakama ya Kibera kufuatia ombi la upande wa mashtaka.

Washukiwa wengine Stephen Oduor na Mercy Gitiri wameachiliwa kwa dhamana ya polisi huku kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tena mwezi Machi 8 mwaka huu.

Upasuaji kwa maiti ya Wanjiku ulibaini kuwa alifariki baada ya kupigwa kichwani kwa kifaa butu.

Wanjiku alitekwa nyara jijini Nairobi na kuuawa kinyama kabla ya mwili wake kutupwa kwenye kichaka huko Kajiado mnamo tarehi 12 mwezi huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here