Kenya yaripoti maambukizi mapya 932 ya ugonjwa wa corona

0

Maambukizi mapya 932 ya ugonjwa wa corona yamedhibitishwa nchini baada ya kupima sampuli 9,424.

Kiwango cha maambukizi nchini kimeshuka na kufikia asilimia 9.9% huku idadi ya visa hivyo ikifikia 233,801.

Wizara ya afya inasema watu wengine 1,457 wamepona na kufikisha idadi hiyo kuwa 218,228.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, idadi ya maafa imeongezeka kwa 31 na kufika 4,666.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here