Mahakama kuu imetaja kama dharura ombi la Polisi sita kutaka miili ya ndugu wawili waliouawa Kianjokoma, kaunti ya Embu kufufuliwa.
Jaji Anthony Mrima ameagiza pande husika kufika mahakamani Jumatano ijayo ambayo ni Septemba 1 kwa maelekezo zaidi.
Sita hao Benson Mputhia, Consolata Kariuki, Nicholas Cheruyoit, Martin Wanyama, Lilian Chemuna na James Mwaniki wanataka uchunguzi wa umma kufanyika kuhusu vifo vya wawili hao kabla ya kushtakiwa kwa mauaji.
Wanataka miili ya wawili hao Benson na Emmanuel Ndwiga kufanyiwa upasuaji mbele yao kwa sababu upasuaji wa kwanza ulifanywa bila wao kuwepo.Kesi