Kenya imepokea msaada wa dozi 880,000 za chanjo ya Moderna kutoka Marekani zilizowasili nchini Jumatatu asubuhi.
Hii ni chanjo ya kwanza aina ya moderna kuwasili nchini chini ya mpango wa kugawa chanjo baina ya mataifa COVAX.
Maafisa wa wizara ya afya wakiongozwa na katibu mkuu wa wizara hiyo Susan Maochache wameongoza shughuli ya kupokea chanjo hiyo.
Mochache amesema watu wenye umri wa zaidi ya miaka 58 wataendelea kupewa kipewa kipau mbele kuchanjwa baada ya data kuonesha kwamba ni walio na umri huo wanafariki kutokana na ugonjwa wa corona.
Dozi hizo zinatazamiwa kupiga jeki juhudi za serikali kuwachanja watu wote wazima humu nchini huku ikilenga watu million kumi kufikia Disemba.
Juma lililopita, Kenya ilipokea dozi 407,000 zaidi za Astrazeneca kutoka nchini Uingereza.
Kenya inatarajiwa kupata dozi 393,000 za Johnson and Johnson na dozi million 1.8 za Pfizer.