Serikali imepiga marufuku sekta ya kibinafsi dhidi ya kusafrishia na kusambaza chanjo ya corona.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema hatua hii inalenga kuhakikisha kuwa kuna uwazei katika shughuli nzima ya kutoa chanjo nchini.
Ameeleza kuwa ni serikali ya Kenya pekee ndiyo ina jukumu la kutoa chanjo ya corona kuanza sasa na kuendelea akionya kuwa watakaokiuka mwongo huo watachukuliwa sheria ikiwemo kupokonywa leseni.
Awali kiongozi wa chama cha Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi alikuwa ameitaka serikali kuwa wazi kuhusu chanjo za AstraZeneca na Sputnik badala ya kuwakanganya Wakenya kuhusu chanjo hizo mbili.