Human Rights Watch lapinga kufungwa kwa kambi za Wakimbizi Kenya

0

Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch (HRW) limeitaka serikali ya Kenya kubatilisha uamuzi wa kufunga kambi za Wakimbizi za Dadaab na Kakuma.

Shirika hilo kupitia taarifa limesema kuwa uamuzi wa kufunga kambi hizo unakwenda kinyume na haki msingi za kibinadamu ambazo Kenya iliahidi kuheshimu.

Human Rights Watch inasema kwa sasa bado wapo Wakimbizi wanaotoroka makwao kutafuta hifadhi Kenya kwa sababu za utovu wa usalama na huu sio wakati mwafaka wa kuwafungia nje.

Wito kama huu umetolewa na shirika la kimataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR ambalo limeitaka Kenya kusitisha mipango ya kufunga kambi hizo zinazotoa hifadhi kwa zaidi ya wakimbizi 500,000.

UNHCR linahoji kwamba kufunga kambi hizo kutakuwa na madhara makubwa wakati huu ambapo ulimwengu unapambana na janga la corona.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here