Kenya yakosa kuripoti maafa yoyote ya corona kwa siku moja

0

Idadi ya maafa kutokana corona nchini imesalia kuwa 1,766 baada ya Kenya kutorekodi kisa chochote cha kifo katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amethibitisha kuwa watu 153 wameambukizwa virusi hivyo na kufikisha idadi ya maambuki nchini kuwa 101,009.

Watu 54 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 83,990.

Wagonjwa 471 wamelazwa katika hospitali mbalimbali  27 wako katika vyumba vya wagonjwa mahututi,12 wanasaidiwa na mashine kupumua.

Msambao wa virusi hivyo ni kama ifuatavyo:Nairobi 93,Mombasa 13, Kiambu 8, Nakuru 6,Turkana 5, Kajiado, Kisumu na Taita taveta 3, Busia, Kirinyaga, Uasin Gishu,Trans Nzoia na Nandi 2

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here