Kenya inatarajiwa kupata chanjo za Pfizer na John & Johnson ili kupiga jeki shughuli ya utoaji wa chanjo inayoendelea kote nchini.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema dozi hizo milioni mbili zitakapofika nchini zitafanikisha shughuli inayoendelea kwa sasa ambapo chanjo ya AstraZeneca imetolewa kwa zaidi ya watu laki saba.
Waziri Kagwe vile vile amewasihi waajiri kujitahidi kuwasaidia wafanyikazi wao waliosimamishwa kazi kutokana na janga la corona.
Na huku taifa likiwa limewapoteza wahudumu wa afya wapatao 38 kutokana na corona, waziri Kagwe amesema wizara hiyo imewapa vifaa vya kujikinga wanapowahudumia wagonjwa.
Wahudumu wa afya walioambikizwa ugonjwa huo ni 4,698 wakiwemo wanawake 2,562 na wanaume 2,136.