Mahakama yatia breki kaunti ya Nairobi kutoza ada mpya za magari jijini

0

Mahakama kuu imeongeza muda wa agizo linaloizuia serikali ya kaunti ya Nairobi dhidi ya kuongeza ada ya kuegesha magari katikati mwa jiji kutoka Sh200 hadi Sh400.

Jaji wa mahakama kuu Anthony Mrima ambaye amerefusha muda wa agizo hilo vile vile ameruhusu shirika linalosimamia Nairobi NMS kujumuishwa kwenye kesi hiyo kama mhusika.

Kesi hiyo itatajwa tena Mei 3 ili kuruhusu pande husika kuwasilisha tetesi zao.

Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na shirika la kutetea haki za watumizi wa bidhaa CofeK pamoja na muungano wa wamiliki wa matatu (MOA) wanaohoji kwamba sio haki kongeza ada hizo pasipo kuhusisha umma.

Ada hizo zilifaa kutozwa magari ya kibinafsi ya umma kuanzia Disemba 4 mwaka jana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here