Mamlaka ya barabara kuu nchini (KENHA) imeomba msamaha wakenya ambao wameathirika na msongamano mkubwa wa magari katika barabara ya Mombasa unaosababishwa na ujenzi wa barabara ya Nairobi Expressway.
Kupitia kwa taarifa, KENHA inasema inashirikiana na maafisa wa trafiki kumaliza msongamano huo haswa kuanzia mtaani Mlolongo hadi katika barabara ya James Gichuru.
KENHA inahoji pia kuwa mvua zinazoendelea kunyesha zimekuwa kizingiti katika ujenzi wa bomba mbadala la kupitisha maji na hivyo kuchangia kuwepo kwa msongamano huo.
Kwa sasa KENHA imeanza ukarabati katika mzunguko wa uwanja wa Nyayo kama njia mojawapo ya kumaliza msongamano.