Maseneta wataka mahakama kuongezwa pesa

0

Maseneta wanataka idara ya mahakama kuongezewa mgao wa bajeti ili kuboresha utendakazi wake.

Wakijadili ombi kutoka kwa mkenya mmoja, aliyeelezea kutoridhishwa kwake na bajeti idara hiyo imetengewa, maseneta wamesema uhaba wa pesa za kutosha kwa idara hiyo umeathiri upatikanaji wa haki.

Itakumbukwa kuwa, aliyekuwa jaji mkuu David Maraga, wakati wa uongozi wake, alililamikia bajeti ya chini ambayo idara hiyo imekuwa ikitengewa ikilinganishwa a idara zingine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here