Chama cha KANU kimejiondoa kwenye uchaguzi mdogo wa wadi ya London kaunti ya Nakuru unaotazamiwa kuandaliwa Alhamisi wiki hii.
Katibu mkuu wa chama hicho Nick Salat amesema uamuzi huo umeafikiwa kuambatana na makubaliano yaliyoafikiwa na chama cha Jubilee.
Haya yanajiri siku chache baada ya chama cha ODM kujiondoa kwenye uchaguzi huo na kusema kitamuunga mkono muwaniaji wa chama cha Jubilee Francis Njoroge alias Njosh.
Kujiondoa kwa KANU na ODM kwenye uchaguzi huo kunamaanisha kuwa kivumbi kitakuwa ni baina ya Jubilee na chama United Democratic Alliance (UDA).
Kiti cha udiwani cha London kilisalia wazi kufuatia kifo cha Samuel Mbugua November, 2020.