Kampeini ya ‘Bila Barakoa, hakuna huduma’ kuzinduliwa Jumatatu ijayo

0

Kuanzia Jumatatu ijayo, baraza la magavana litaanzisha kampeini ya ‘Bila Barakoa, Hakuna Huduma’ kutoa hamasisho kwa Wakenya kuzingatia masharti ya usalama kuzuia msambao wa virusi vya corona.

Mwenyekiti wa baraza hilo Wycliff Oparanya anasema Jumanne kwa ushirikiano na makamishna wa kaunti wataanzisha mikakati itakayohakikisha kuwa masharti hayo yametekelezwa kikamilifu.

Oparanya vile vile amesema serikali za kaunti zinajitahidi kuwalinda wahudumu wa afya pamoja na familia zao iwapo wataambukizwa virusi hivyo vya corona kwani wako katika mstari wa mbele kupambana na ugonjwa huo.

Baraza hilo aidha limeitaka serikali kuu kuharakisha kutuma pesa za kaunti kwani kwa miezi mitatu sasa pesa hizo zimecheleweshwa na hivyo kuhujumu utoaji hudumu katika serikali za kaunti.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here