Sakata ya Ruaraka: Itumbi amshtaki Matiang’i

0

Mwanablogu Dennis Itumbi amemshtaki waziri wa usalama wa ndani Dkt. Fred Matiang’i kuhusiana na sakata ya ardhi ya Ruaraka.

Itumbi kwenye kesi yake katika mahakama ya kupambana na ufisadi ya Milimani anahoji kuwa Wakenya walipoteza hadi Sh1.5b kupitia ulipaji fidia ambao haukufuata sheria.

Mwanablogu huyo anadai kuwa Matiang’i ambaye alikuwa waziri wa elimu wakati huo aliidhinisha ulipaji wa fidia hiyo kwa watu binafsi licha ya kushauriwa kuwa ardhi hiyo ambapo shule ya msingi ya Drive In na shule ya upili ya Ruaraka zimejengwa ni ya serikali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here