Jela miaka 30 kwa jamaa aliyemkata mkewe mikono

0

Mwanaume aliyemkata mkewe Jackline Mwende mikono amepewa kifungu cha miaka 30 jela na mahakama ya Machakos.

Hakimu mkuu mkaazi Brenda Bartoo ametoa uamuzi huo baada ya mtuhumiwa Stephen Ngila kuhusika kwenye jaribio la mauaji Julai tarehe 25 mwaka 2016 katika kaunti ya Machakos.

Aidha mahakama imempa Ngila siku 14 kukata rufaa iwapo hajaridhishwa na uamuzi huo.

Mwende amewaambia wanahabari kwamba mumewe alimshambulia kwa sababu alikuwa ameshindwa kupata watoto.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here