JAJI MKUU KOOME APUUZILIA MATAMSHI YA RUTO KUHUSU MAKUBALIANO NA MAHAKAMA

0
PRESIDENT RUTO AND CJ KOOME
PRESIDENT RUTO AND CJ KOOME

Jaji mkuu Martha Koome ameitetea idara ya mahakama akisema kuwa hakuna maelewano yoyote kati ya serikali kuu na idara ya mahakama kama alivyotangaza Rais William Ruto wikendi iliyopita.

 

Msimamo wa Koome ukifuatia matamshi ya Rais alipokuwa Bomet kuwa wamekubaliana na mahakama kuhusu ushuru wa nyumba.

 

“Hatujaafikiana chochote na Rais. Kama Idara ya mahakama hatuna uwezo wa kuafikiana chochote na idara tendaji ya serikali kuhusu swala lililo mahakamani.” Amesema Koome.

 

Akizungumza mjini Bomet Rais William Ruto alidai kuwa waliafikia makubalino na mahakama kuhusu ujenzi wa nyumba za bei nafuu.

 

Jaji Mkuu ambaye sawia ni Rais wa Mahakama ya Upeo amesema huenda matamshi ya kiongozi wa taifa yalitafsiriwa visivyo.

 

“Mimi sio mtaalamu wa mawasialiano lakini nahisi kuwa huenda Matamshi ya Rais yaliondolewa kutoka kwa muktadha wake.” Alisema Koome.

 

Haya yanajiri huku Mahakama kuu ikidinda kusitisha utekelezaji wa sheria mpya ya nyumba za nafuu,

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here