KAMISHNA WA KAUNTI YA LAMU LOUIS RONO AAGA DUNIA

0
LAMU COMMISIONER RONO
LAMU COMMISIONER RONO

Kamishna wa Kaunti ya Lamu Loius Rono ameiga dunia; ametangaza waziri wa usalama Kindiki Kithure.

Katika taarifa yake, Kindiki amesema Rono alitumikia nchi kwa uzalendo na kujitolea kwa miaka 28 pasi na kutajwa kwenye kashfa yoyote.

Alibainisha kuwa marehemu kamishna wa kaunti atakumbukwa kwa kuongoza kikosi cha Usalama na Ujasusi cha Kaunti ya Lamu katika vita dhidi ya ugaidi katika Msitu wa Boni.

“Jioni ya leo, tunajipata katika hali ya huzuni tunapomkumbuka Louis Kipngetich Ronoh, Kamishna wa Kaunti ya Lamu, ambaye ameondoka kwa huzuni kufuatia kuugua kwa muda mfupi.” Taraifa ya waziri Kindiki imesema

Katibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Raymond Omollo ameomboleza kifo cha Ronoh na kumtaja kama afisa aliyekuwa na  bidi kazini

“Ni kwa huzuni kubwa kwamba nimejuzwa  kuhusu kifo cha Louis Kipngetich Ronoh, baada ya kuugua kwa muda mfupi,” alisema.

“Marehemu Ronoh atakumbukwa kwa kujitolea kwake katika kuwatumikia wengine na nchi. Mawazo na sala zetu ziko pamoja na familia yake na marafiki,” Omollo aliongeza.

Mbunge wa Lamu Magharibi Stanley Muthama alisema marehemu alikuwa sehemu muhimu ya jamii katika masuala ya usalama, ushirikishwaji wa umma, amani, utangamano na utangamano.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here