IEBC yaonya upungufu wa ufadhili wa Ksh33B unaweza kuathiri uchaguzi wa 2027.

0

Maaafisa wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka nchini IEBC wamefika mbele ya kamati ya Haki na Masuala ya Kisheria ya Bunge la Kitaifa kujadili makadirio ya bajeti ya kufanikisha uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Wabunge wamehimizwa na maafisa hao kuhakikisha IEBC inapata mgao wa fedha za kutosha kwa sababu idadi ya wapiga kura inatarajiwa kuongezeka hadi zaidi ya milioni 28 tofauti na milioni 22 mwaka 2022.

” Tunatarajia kuwa na wapiga kura waliosajiliwa milioni 28.5 katika uchaguzi mkuu wa 2027, ikilinganishwa na wapiga kura milioni 22.1 waliosajiliwa mwaka 2022. Kulingana na takwimu hizo, na kwa kuzingatia idadi ya vituo vya kupigia kura vinavyotarajiwa, tutakuwa na wastani wa watu 500 kwa kila kituo cha kupigia kura. ” imesema tume hiyo.

Aidha Tume hiyo inahitaji Takriban shilingi bilioni 74 ili kuendesha uchaguzi mkuu huru na wa haki nchini ikionya kuwa kuna upungufu wa shilingi bilioni 33 unaoweza kuathiri utekelezaji wa shughuli za uchaguzi

IEBC imeeleza kuwa hadi kufikia sasa imepokea mgao wa shilingi bilioni 41 na kwamba fedha hizo bado hazitoshi kukamilisha maandalizi yote muhimu ya uchaguzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here