ICJ wapinga marekebisho ya katiba kupitia BBI

0

Muungano wa mawakili (ICJ) tawi la Kenya umetangaza kuwa kupinga marekebisho ya katiba kupitia kwa BBI.

Katika taarifa, mwenyekiti wa muungano huo Kelvin Mogeni anasema mapendekezo yaliyo kwenye mswada wa marekebisho ya katiba mwaka 2020, yanalenga kurudisha nyuma hatua zilizopigwa kufikia sasa tangu mwaka 2010.

Mogeni anasema kwa mfano, pendekezo la kuwa na afisi ya Ombudsman katika idara ya mahakama ni kuhujumu uhuru wa idara hiyo.

Mogeni anasema BBI haina nia njema ya kusuluhisha shida zinazowakumba wakenya ikiwemo pia kuleta uwakilishi sawa wa jinsia.

Wakati uo huo

Msemaji wa serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna amewasihi wakenya kuunga mkono ripoti ya BBI akisema mapendekezo ya ripoti hiyo yanalenga kumaliza migogoro inayoibuka kila baada ya uchaguzi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here