Hisia zatolewa kuhusu kusimamishwa kwa BBI

0

Uamuzi  wa mahakama kuu uliosimamisha ubadilishaji wa katiba kupitia mchakato wa BBI unaendelea kupokelewa kwa hisia mbalimbali.

Kamati ya BBI ikiongozwa na mwenyekiti mwenza Junet Mohamed imesema itakata rufaa wiki ijayo.

Mohamed amesema kwamba wataendelea kupigia debe mchakato wa BBI  na hawakubaliani na maamuzi ya hapo jana.

Naye…..

Naibu rais William Ruto ametaja uamuzi huo kama unaolenga kulinda katiba na sheria.

Ruto kupitia mtandao wake wa Twitter amesema sawa na ilivyofanya idara ya mahakama, kila Mkenya mzalendo ana jukumu la kulinda katiba na sheria.

Naibu rais ambaye hajapinga mchakato wa BBI moja kwa moja sasa anasema ni wakati wa kuangazia zoezi la kutoa chanjo ya corona kwa Wakenya, kuinua uchumi uliokwama kufuatia corona na ajenda NNE za serikali.

Kwa upande wake

Kiongozi wa chama cha Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi amekosoa uamuzi akisema huenda siasa zilihusishwa katika kutoa uamuzi huo.

Katika uamuzi huo, majaji watano walisema swala nzima la kubadilisha katiba linaendeshwa kinyume na sheria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here