“Hatutakuruhusu uturejeshe 2007-08” Msemaji wa serikali aonya Gachagua.

0
Msemaji wa serikali Issac Mwaura

Msemaji wa serikali Issac Mwaura amelaani matamshi ya aliyekuwa naibu wa Rais kuhusu uwezekano wa vurugu baada ya uchaguzi wa mwaka 2027.

Akizungumza wakati wa kikao na vyombo vya habari Dkt. Mwaura amesema kauli ya Gachagua wakati wa mahojiano kwenye kipindi cha “Obinna Show” yananuia kugawanya nchi.

“Inasikitisha kwa viongozi kuchochea umaa ili kupata umaarufu wa kisiasa. Tusisahau kwamba malfunction waliaga dunia mwaka wa 2007 hatutasaza chochote kuhakikisha usalama wa taifa”. Amesema Mwaura.

Gachagua katika mahojiano hayo alidai kwamba huenda taifa likasambaratika iwapo tume ya uchaguzi IEBC itahitilafiana na uchaguzi mkuu ujao.

“Hatutakua na nchi iwapo uchaguzi utaingiliwa, 2007-08 utaonekana kama mzaha.” Gachagua alihoji.

Msemaji wa serikali sawia amepuuzilia mbali madai kwamba kiongozi wa taifa Rais William Ruto amejilimbikizia zaidi ya sh. Trillioni 4 katika kipindi cha miaka miwili.

Msemaji wa serikali ameongeza kuwa wanaoeneza kile ametaja kama number potovu hawafurahii hatua zilizopigwa na utawala wa Rais Ruto.

Kwingine Gachagua kupitia wakili wake Ndegwa Njiru amedai kwamba makachero wa idara ya upelelezi wa makosa ya Jinai wanamuandamana wakinuia kumtia mbaroni.

Kiongozi huyo wa chama cha DCP amedokeza kwamba maafisa hao usiku wa kuamkia leo walizingira makazi yake ya Karen na Wamunyoro.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here