Hatimaye matabibu wasitisha mgomo wao kufuatia agizo la mahakama

0

Hatimaye matibabu wamesitisha mgomo wao uliodumu kwa zaidi ya miezi mitatu baada ya mahakama kuwaamrisha kurejea kazini.

Jaji wa mahakama ya Leba Maureen Onyango amewaagiza matabibu warudi kazini haraka iwezekanavyo huku akiagiza walipwe mishahara yao.

Mwenyekiti wa muungano wa matabibu nchini (KUCO) Peter Wachira amewataka wahudumu hao wa afya kuripoti kazini licha ya kwamba malalamishi yao bado hayajashughulikiwa.

Katika kaunti ya Busia, wahudumu wa afya wamesitisha mgomo wao baada ya kuafikia maelewano na serikali ya kaunti hiyo.

Gavana wa Busia Sospeter Ojamong’ amesema wahudumu hao wamekubali kurudi kazini bila masharti yeyote.

Itakumbukwa kwamba wauguzi pamoja na matabibu waligoma katika muda wa siku sabini na mbili zilizopita wakilalamikia maswala mbalimbali ikiwemo mishahara pamoja na kupandishwa vyeo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here