Haki za watu wenye mahitaji maalum katika jamii zimekiukwa tangu taifa lilipoanza kupambana na janga la kimataifa la corona.
Utafiti wa hivi punde uliotolewa na tume ya kitaifa ya kutetea haki za kibinadamu (KNCHR) umebaini kuwa watu hao wakiwemo walemavu, vijana, wazee na akina mama walikosa kupata huduma za matibabu na pia kukatiwa maji.
Utafiti huo umebaini kuwa asilimia kubwa ya watu hao walifukuzwa katika nyumba zao kwa kushindwa kulipa kodi na hivyo kuwaacha bila mahala pa kuishi.
Aidha, asilimia 67% ya waliohojiwa wanasema walikosa kupata chakula na hivyo kulazimika kutegemea chakula cha msaada.
Katika mapendekezo yake, tume hiyo kupitia afisa mkuu mtendaji Benard Mogesa inaitaka serikali kushughulikia changamoto ya kupanda kwa gharama ya maisha ili kuwaokoa Wakenya.
Utafiti huo ulifanywa na kampni ya Infotrack kati ya Julai 2020 na Machi 2021.