Haijalishi Mgombea Mwenza Msimamo wa Mlima Kenya Ni Kumuunga Mkono Ruto: Waziri Afichua.

0

Waziri wa Utumishi wa Umma Geofrey Ruku amesema eneo la Mlima Kenya hasa Mlima Kenya Mashariki litaendelea kumwunga mkono Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 hata kama hatamteua tena Naibu wake wa sasa Profesa Kithure Kindiki kuwa mgombea mwenza.

Akizungumza Mnamo Julai 27 2026, Ruku amesema uteuzi wa mgombea mwenza ni mamlaka ya Rais na kwamba wafuasi wa Kenya Kwanza wanapaswa kuheshimu uamuzi wowote atakoufanya

Hata hivyo Ruku amesema anamwunga mkono Kindiki kuendelea kuhudumu kuwa Naibu wa Rais akisema ameonyesha utendakazi mzuri katika nafasi hiyo na kwamba anafaa kuendelea kusalia ofisini hadi mwaka 2032

“Ninamuunga mkono Kindiki kuendelea kuwa Naibu Rais kwa sababu amefanya vizuri sana kama msaidizi wa Ruto. Ameonyesha Utendakazi mzuri kama Naibu Rais, na nadhani anafaa kuwa Naibu Rais kuanzia 2027 hadi 2032,” Ruku alisema.

“Ikiwa hatachaguliwa, tutaendelea kumuunga mkono Rais Ruto. Ni haki ya mkuu wa nchi kuchagua mgombea mwenza wake,” aliongeza.

Kauli ya Ruku inajiri baada ya viongozi wa chama cha ODM kupendekeza Waziri wa Vyama vya Ushirika Wycliffe Oparanya kuwa Mgombea Mwenza wa Rais Ruto katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2027.

Kulingana na ODM, nafasi ya Naibu Rais inapaswa kutengwa kwa ajili ya chama hicho, ikizingatiwa kwamba chama cha UDA tayari kina mgombea urais ambaye wote wanamuunga mkono.

Wakiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu Catherine Omanyo, viongozi hao walisisitiza kwamba kufuatia maelewano ndani ya serikali jumuishi wanatarajia kupewa nafasi hiyo ya Naibu Rais.

“UDA inapaswa kupeana Rais huku ODM ikipeana Naibu wake nasi tutamwasilisha Wycliffe Oparanya,” Junet Mohamed alisema wakati wa mkutano huko Malava.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here